• HABARI MPYA

  Saturday, February 18, 2023

  NYOTA WA GHANA, CHRISTIAN ATSU AFARIKI DUNIA UTURUKI


  MWILI wa mwanasoka wa Ghana Christian Atsu umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi kusini mwa Uturuki baada ya tetemeko kubwa la ardhi wiki iliyopita.
  Wakala wa winga huyo wa zamani wa Chelsea amenukuliwa na Reuters akielezea kifo cha nyota huyo wa Ghana ambaye alikuwa anachezea Hatayspor ya Ligi Kuu ya Uturuki.
  "Mwili wa Atsu ulipatikana chini ya vifusi," Murat Uzunmehmet aliwaambia waandishi wa habari huko Hatay, ambapo mwili wa mwanasoka huyo ulipatikana.
  "Kwa sasa, vitu zaidi bado vinatolewa. Simu yake pia ilipatikana." 
  Atsu alikuwa amepanga kusafiri Kusini mwa Uturuki saa chache kabla ya tetemeko hilo kutokea, lakini alisema Ijumaa Mghana huyo aliamua kusalia na klabu hiyo baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi ya Februari 5 ya ligi ya Uturuki (Super Lig).
  Atsu aliwahi kuichezea Newcastle United pia. Mungu ampumzishe kwa amani. Amin.
  WASIFU WA MAREHEMU CHRISTIAN ATSU
  Jina KamiliChristian Atsu Twasam[1]
  Tarehe ya Kuzaliwa10 January 1992
  Mahali AlipozaliwaAda Foah, Ghana
  Tarehe ya Kifo chakec. 6 February 2023(aged 31)
  Mahali Alipofia Antakya, Turkey
  Ukubwa wa mwili1.65 m (5 ft 5 in)[2]
  Nafasi aliyekuwa anachezaWinga
  Timu za Vijana
  Feyenoord Fetteh
  Cheetah
  2009–2011Porto
  Timu za Wakubwa
  MwakaTimuMechi(Mabao)
  2011–2013Porto17(1)
  2011–2012→ Rio Ave (loan)27(6)
  2013–2017Chelsea0(0)
  2013–2014→ Vitesse (loan)28(5)
  2014–2015→ Everton (loan)5(0)
  2015–2016→ Bournemouth (loan)0(0)
  2016→ Málaga (loan)12(2)
  2016–2017→ Newcastle United (loan)32(5)
  2017–2021Newcastle United75(3)
  2021–2022Al-Raed8(0)
  2022–2023Hatayspor3(1)
  Total207(23)
  Timu ya Taifa
  2012–2019Ghana65(9)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NYOTA WA GHANA, CHRISTIAN ATSU AFARIKI DUNIA UTURUKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top