• HABARI MPYA

  Saturday, February 18, 2023

  ARSENAL YATOKA NYUMA MARA MBILI KUSHINDA 4-2


  TIMU ya Arsenal imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Aston Villa leo Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Haukuwa mshindi mwepesi kwa Washika Bunduki hao, kwani mara mbili walilazimika kutoka nyuma kabla ya kupata mabao mawili ya ushindi dakika za majeruhi.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 16, Oleksandr Zinchenko dakika ya 61, Emiliano Martínez aliyejifunga dakika ya tatu ya nyongeza baada ya kutimia 90 za kawaida na  Gabriel Martinelli dakika ya nane ya muda wa nyongeza.
  Kwa upande wao Aston Villa walioanza vizuri mchezo wa leo kabla ya kupoteza mwishoni, mabao yao yamefungwa na Ollie Watkins dakika ya tano na Philippe Coutinho dakika ya 31.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 54 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 28 za mechi 23 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YATOKA NYUMA MARA MBILI KUSHINDA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top