• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2023

  M-BET YAMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WAWILI, YAIOMBEA HERI SIMBA


  KAMPUNI ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imewazawadia washindi wawili kila mmoja Sh175.3 millioni baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12.
  Washindi hao ni Mesharam Bakunda na Abdallah Segatwa ambao walizawadiwa fedha zao jana katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni ya M-BET Tanzania jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania Allen Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadili maisha ya mashabiki hao wa soka ambao wote ni wafuasi wa klabu ya Arsenal.
  Mushi alisema kuwa washindi hao wawili wanaungana na wengine wengi katika nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kujaribu bahati zao kwa kubashiri na kampuni yao.
  “Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia  asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja serikalini . Sisi ni walipa kodi wazuri wa serikali na tunachangia maendeleo,” alisema Mushi ambaye pia ameitakia Simba mafanikio mema katika mchezo wake na Vipers ya Uganda utakaochezwa leo.
  Kwa upande wake, Bakunda ambaye pia ni shabiki wa Yanga alisema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1, 000 tu.  Alisema kuwa amekuwa akibashiri na M-BET mara kwa mara kwani ameshuhudia washindi kadhaa wakishinda fedha nyingi kupitia kampuni hiyo.
  Naye Segatwa alisema kuwa hakukata tamaa katika safari yake ya kubashiri na mara kadhaa alikuwa anabashiri na kushinda fedha kidogo.
  “Mimi mkulima, nitatumia fedha hizi kwa ajili ya kuendelza kilimo, kuboresha nyumba na kusomesha watoto wangu. Nimekuwa nikibashiriki na kupata hela ndogo ndogo. Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini  na nilidhani ni ndoto,” alisema Segatwa.


  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania Allen Mushi (Kulia) akimkabidhi mfano wa hundi  yenye thamani ya sh 175.3 millioni Mesharam Bakunda aliyeshinda kitita cha fedha hicho kupitia droo ya Perfect 12.
  Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania Allen Mushi (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi  yenye thamani ya sh 175.3 millioni Abdallah Segatwa aliyeshinda kitita cha fedha hicho kupitia droo ya Perfect 12.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: M-BET YAMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WAWILI, YAIOMBEA HERI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top