• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2023

  BENKI YA NBC YAIKOPESHA KMC BASI LA SH MILIONI 450


  BENKI ya NBC ambaye ni Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premier League hii leo imekabidhi basi jipya kwa timu ya KMC FC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alishuhudia tukio hilo na kupongeza jitihada za Benki ya NBC katika kuboresha Ligi Kuu ya NBC.
  Hafla ya makabidhiano ya basi hilo lenye thamani ya sh ya milioni 450 lililotolewa kama mkopo kutoka Benki ya NBC imefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali. 
  Pamoja na RC Makalla, wakikuwepo Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kindondoni wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Saad Mtambule.
  Akizungumza kwenye hafla hiyo RC Makalla, aliipongeza Benki ya NBC kwa jitihada za kuiboresha ligi hiyo kimataifa huku akitoa wito kwa vilabu mbalimbali nchini kuitumia vema kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo mikopo ya usafiri na Bima kwa wachezaji na benchi la ufundi.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BENKI YA NBC YAIKOPESHA KMC BASI LA SH MILIONI 450 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top