• HABARI MPYA

  Saturday, February 04, 2023

  YANGA SC YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 DAR


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na beki wa Kimataifa wa Tanzania, Dickson Job dakika ya 43 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 51.
  Kwa ushindi huo timu ya Wananchi inafikisha pointi 59 na kuendelea kuongoza ligi kwa pointi sita zaidi ya mtani, Simba baada ya wote kucheza mechi 22.
  Kwa upande wao Namungo FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 29 za mechi 22 pia nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top