• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2023

  YANGA YAENDA TUNISIA KUMENYANA NA MONASTIR


  KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Monastir Jumapili kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Olympique Hammadi Agrebi mjini Radès, Tunis.
  Baada ya mchezo huo, Yanga itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo wa pili Februari 19 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi hilo mzunguko wa kwanza kwa kukipiga na wenyeji, Real Bamako nchini Mali Februari 26.
  Mzunguko wa pili Yanga itaanza nyumbani dhidi ya Real Bamako Mechi 8, kabla ya kuwapokea Monastir Machi 19 na kwenda kukamilisha mechi za kundi hilo Jijini Lubumbashi mbele ya TP Mazembe Aprili 2.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAENDA TUNISIA KUMENYANA NA MONASTIR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top