• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2023

  NAMUNGO FC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 RUANGWA


  WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
  Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Relliant Lusajo dakika ya 21 na Parterne Counou dakika ya 47, wakati la Geita Gold limefungwa na Elias Maguri dakika ya 64.
  Kwa ushindi huo Namungo FC inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya saba, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 34 nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 RUANGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top