• HABARI MPYA

  Tuesday, February 07, 2023

  SIMBA YAZINDUA JEZI ZA LIGI YA MABINGWA


  KLABU ya Simba imezindua jezi maalum kwa ajili ya Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambazo zimebeba ujumbe wa kuitangaza Tanzania.
  Simba itacheza mechi yake ya kwanza ya Kundi C Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji, Horoya Jumamosi Uwanja wa Jénérali Lansana Conté Jijini Conakry, Guinea.
  Baada ya hapo, Simba itarejea nyumbani kwa mchezo wa pili dhidi ya Raja Casablanca Februari 18, kabla ya kwenda kukamilisha mzunguko wa kwanza kwa kumenyana na Vipers ya Uganda Februari 25 Uwanja wa St. Mary's, Kitende mjini Entebbe.
  Mechi za mzunguko wa pili Simba itaanzia nyumbani dhidi ya Vipers Machi 7, kabla ya kuwakaribisha Horoya Machi 17 na kuwafuata Raja Casablanca Machi 31.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAZINDUA JEZI ZA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top