• HABARI MPYA

  Monday, February 27, 2023

  BAKHRESA GROUP, AZAM MEDIA NI SUPER BRANDS


  KAMPUNI ya Azam Media pamoja na Kampuni mama ya Bakhresa Group zimeng’ara kwenye tuzo za Super Brands (Chaguo la Afrika Mashariki) kwa mwaka 2022 – 2024.
  Tuzo hizo zimekabidhiwa kwa kampuni hizo na waandaji wa tuzo hizo katika ofisi za Azam Media zilizopo, Tabata, Dar es Salaam.
  Kwa upande wa Azam Media na Bakhresa Group tuzo hizo zilipokelewa na Afisa Uhusiano wa Bakhresa Group, Rehema Salim na Mhariri wa Dawati la Habari na Matukio wa Azam media, Ben Mwang’onda.
  Jumla ya kampuni nane zimepokea tuzo hiyo na kukabidhiwa kwao na Mkurugenzi wa Mradi wa Superbrand, Jawad Jaffer.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAKHRESA GROUP, AZAM MEDIA NI SUPER BRANDS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top