• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2023

  MAN UNITED WATWAA TAJI LA KWANZA BAADA YA MIAKA SITA


  TIMU ya Manchester United imefanikiwa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle United leo Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Casemiro dakika ya 33 na Sven Botman aliyejifunga dakika ya 39 baada ya kubabatizwa na mpira uliopigwa na Marcus Rashford na hilo linakuwa taji la kwanza kwa Mashetani hao Wekundu tangu mwaka 2017.
  Linakuwa taji la kwanza kwa kocha mpya, Mholanzi Erik ten Hag katika msimu wake wa kwanza tu Manchester United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED WATWAA TAJI LA KWANZA BAADA YA MIAKA SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top