• HABARI MPYA

  Sunday, February 12, 2023

  IHEFU YAAMBULIA SARE 1-1 NA SINGIDA BIG STARS MBARALI


  WENYEJI, Ihefu SC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya.
  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, mzaliwa wa Uganda , Meddie Kagere alianza kuifungia Singida Big Stars dakika ya 63, kabla ya mshambuliaji Mburkinabe,Yacouba Sogne kuisawazishia Ihefu dakika ya 72.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya nane, ikizidiwa pointi mbili na Mtibwa Sugar baada ya wote kucheza mechi 23.
  Kwa upande wao Singida Big Stars inafikisha pointi 44 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya tatu ikiizidi pointi moja Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU YAAMBULIA SARE 1-1 NA SINGIDA BIG STARS MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top