• HABARI MPYA

  Sunday, February 12, 2023

  MAN CITY YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 ETIHAD


  MABINGWA watetezi, Manchester City FC wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa FC leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Rodri dakika ya nne, Ilkay Gündoğan dakika ya 39 na Riyad Mahrez kwa penalti dakika ya 45, wakati la Aston Villa limefungwa na Ollie Watkins dakika ya 61.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 48 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Aston Villa wanabaki na pointi zao 28 za mechi 22 nafasi ya 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAICHAPA ASTON VILLA 3-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top