• HABARI MPYA

  Sunday, February 05, 2023

  SIMBA SC NA AL HILAL NGUVU SAWA, SARE 1-1


  WENYEJI, Simba SC wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal ya Sudan katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Hilal ya kocha Florent Ibenge ilitangulia kwa bao la mshambuliaji Mkongo mwenzake, Glody Makabi Lilepo dakika ya sita kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Habib Kyombo kuisawazishia Simba SC dakika ya 81.
  Hilal imekamilisha kambi yake ya kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa Ligi ya Mabingwa Afrika wiki ijayo dhidi ya wenyeji, Mamelodi Sundowns bila kupoteza katika mechi tatu za kirafiki.
  Ilianza kwa sare na Namungo 1-1, kabla ya kuifunga Azam FC 1-0 na leo imefunga biashara kwa sare nyingine ya 1-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC NA AL HILAL NGUVU SAWA, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top