• HABARI MPYA

  Saturday, February 04, 2023

  DODOMA JIJI YAICHAPA 2-1 AZAM FC PUNGUFU


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Muhsin Makame dakika ya 26 na Collins Opare dakika ya 30, wakati la Azam FC limefungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 60.
  Azam FC ilimaliza pungufu baada  ya beki wake Msenegal, Malickou Ndoye kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 42.
  Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji wanafikisha pointi 24 na kusogea nafasi ya 10, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 43 nafasi ya tatu baada ya wote kucheza mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA 2-1 AZAM FC PUNGUFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top