• HABARI MPYA

  Thursday, February 16, 2023

  MAN CITY YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA ARSENAL 3-1


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa, Arsenal usiku wa jana Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Mabao ya Manchester City yalifungwa na Kevin De Bruyne dakika ya 24, Jack Grealish dakika ya 72 na Erling Haaland dakika ya ambalo linakuwa bao lake la 32, wakati la Arsenal lilifungwa na Bukayo Saka kwa penalti dakika ya 42.
  Kwa ushindi huo wa ugenini, Manchester City wanafikisha pointi 51 katika mchezo wa 23 na kupanda juu ya msimamo, wakiizidi Arsenal wastani tu wa mabao, ingawa Washika Bunduki wa London wana mechi moja mkononi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAREJEA KILELENI BAADA YA KUICHAPA ARSENAL 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top