• HABARI MPYA

  Wednesday, February 01, 2023

  AZAM FC YAINGIA MKATABA NA AGA KHAN


  KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya matibabu ya wachezaji na wafanyakazi wake wote.
  Taarifa ya Azam FC imesema kwamba mkataba huo wa miaka miwili umesainiwa leo katika hospitali hiyo iliyopo eneo la Sea View Upanga Dar Es Salaam.
  Mtendaji mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Nurdin Mohamed Amin 'Popat' na mwenzake Sisawo Konteh wa Aga Khan ndiyo waliosaini mkataba huo kwa niaba ya taasisi zao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAINGIA MKATABA NA AGA KHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top