• HABARI MPYA

  Sunday, February 05, 2023

  KANE AFUNGA BAO LA REKODI SPURS YAIPIGA MAN CITY 1-0


  WENYEJI, Tottenham Hotspur wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Nahodha Harry Kane dakika ya 15 akimalizia pasi ya kiungo Mdenmark, Pierre-Emile Højbjerg hivyo nyota huyo wa England akivunja rekodi ya ufungaji bora wa muda wote Spurs kwa kufikisha mabao 267 na kumpiku Jimmy Greaves.
  Kwa ushindi huo, Tottenham Hotspur inafikisha pointi 39 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi moja na Newcastle United ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Manchester City baada ya kipigo hicho mbele ya Spurs iliyomaliza pungufu leo kufuatia beki wake Muargentina, 
  Cristian Gabriel Romero kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 87 inabaki na pointi zake 45 za mechi 21 nafasi ya pili nyuma y Arsenal yenye pointi 50 za mechi 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KANE AFUNGA BAO LA REKODI SPURS YAIPIGA MAN CITY 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top