• HABARI MPYA

  Sunday, February 12, 2023

  MAN UNTIED YAILAZA LEEDS UNITED 2-0 ELLAND ROAD


  MABAO ya Marcus Rashford dakika ya 80 na Alejandro Garnacho dakika ya 85 leo yameipa Manchester United ushindi wa 2-0 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Elland Road mjini Leeds, West Yorkshire.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 46 katika mchezo wa 23, ingawa inabaki nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi mbili na Manchester City ambayo pia ina mechi moja mkononi, wakati Leeds United inabaki na pointi zake 19 za mechi 22 nafasi ya 17.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNTIED YAILAZA LEEDS UNITED 2-0 ELLAND ROAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top