• HABARI MPYA

  Tuesday, February 14, 2023

  SALAH AFUNGA LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0


  MABAO ya washambuliaji Mmisri, Mohamed Salah dakika ya 36 na Mholanzi, Cody Gakpo dakika ya 49 jana yaliipa Liverpool ushindi wa 2-0 dhidi ya mahasimu, Everton FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Everton inabaki na pointi zake 18 za mechi 22 nafasi ya 18.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALAH AFUNGA LIVERPOOL YAICHAPA EVERTON 2-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top