• HABARI MPYA

    Saturday, February 04, 2023

    EVERTON YAIPUNGUZA KASI ARSENAL, YAICHAPA 1-0


    BAO pekee la beki James Alan Tarkowski dakika ya 60 limeipa Everton ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool.
    Kwa ushindi huo, Everton inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya 17, wakati Arsenal inabaki na pointi zake 50 ikiendelea kuongoza ligi kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 20.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EVERTON YAIPUNGUZA KASI ARSENAL, YAICHAPA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top