• HABARI MPYA

  Saturday, February 04, 2023

  MAN UNITED PUNGUFU YAICHAPA CRYSTAL PALACE 2-1


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Man United yamefungwa na Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya saba na Marcus Rashford dakika ya 62, wakati la Crystal Palace limefungwa na Jeffrey Schlupp dakika ya 76.
  Manchester United ilimaliza pungufu baada ya kiungo wake Mbrazil, Carlos Casimiro kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 70 kufuatia kumsukuma hadi nje ya Uwanja kiungo Mghana mzaliwa wa Ujerumani Jeffrey Schlupp.
  Casimiro alifanya hivyo kulipa kisasi baada ya Schlupp kumuangushia nje ya Uwanja Mbrazil mwenzake, Antony.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 42 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidwa pointi tatu na jirani zao, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Crystal Palace baada ya kupoteza mechi ya leo wanabaki na pointi zao 24 za mechi 21 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED PUNGUFU YAICHAPA CRYSTAL PALACE 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top