• HABARI MPYA

  Wednesday, February 22, 2023

  MZIZE APIGA BAO PEKEE YANGA YASHINDA 1-0


  BAO pekee la mshambuliaji chipukizi, Clement Mzize dakika ya 38 limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 62 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi nane zaidi ya watani, Simba baada ya wote kucheza mechi 23.
  Kwa upande wao, KMC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 23 za mechi 23 pia nafasi ya 12 kwenye ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MZIZE APIGA BAO PEKEE YANGA YASHINDA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top