• HABARI MPYA

  Tuesday, February 14, 2023

  BALOZI PINDI CHANA WAZIRI MPYA WA MICHEZO


  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dk. Pindi Hazara Chana kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  Dk. Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii anachukua nafasi ya Mohamed Omary Mchengerwa aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  Mabadiliko hayo yanampeleka Mchengerwa Wizara ya Maliasili na Utalii.
  Rais Samia pia amemuhamishia Dkt. Hassan Abbas Said, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua anachukua nafasi ya Profesa Eliamani M. Sedoyeka.
  Rais Samia pia amemteua Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akichukua nafasi ya Dkt. Hassan Abbas Said, Kabla ya uteuzi huo, Yakub alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.   • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BALOZI PINDI CHANA WAZIRI MPYA WA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top