• HABARI MPYA

  Friday, February 03, 2023

  SIMBA SC YAITANDIKA SINGIDA BIG STARS 3-1 DAR


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mkongo Jean Baleke dakika ya nane, kiungo Mrundi Saido Ntibanzokiza dakika ya 21 na winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 35.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 53 katika mchezo wa 22, ingawa inasalia nafasi ya pili ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao Singida Big Stars ambayo bao lake lilifungwa kiungo Mbrazil, Bruno Gomes dakika ya 35, baada ya kupoteza mchezo wa leo inabaki na pointi zake 43 za mechi 22 nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA SINGIDA BIG STARS 3-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top