• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2023

  MAYELE AFUNGA YANGA YATOA DROO MALI 1-1


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC leo wamelazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Real Bamako Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.
  Yanga walitangulia na bao la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 60, kabla ya beki mzawa, Émile Koné kuisawazishia Real Bamako dakika ya 90 na ushei.
  Mechi nyingine ya Kundi D leo, Monastir ya Tunisia imepata ushindi wa ugenini wa 2-0 dhidi ya wenyeji, TP Mazembe Uwanja wa Mazembe Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Sasa Monastir inaendelea kuongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Yanga pointi nne, Mazembe tatu na Real Bamako mbili.
  Mechi zijazo Machi Yanga watakuwa wenyeji wa Real Bamako Jijini Dar es Salaam na Monastir watawakaribisha Mazembe Jijini Tunis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE AFUNGA YANGA YATOA DROO MALI 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top