• HABARI MPYA

  Saturday, February 25, 2023

  MAN CITY YAIFUMUA BOURNEMOUTH 4-1 VITALITY


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality Jijini Bournemouth, Dorset.
  Mabao ya Manchester City yamefungwa na Julian Alvarez dakika ya 15, Erling Haaland dakika ya 29, Phil Foden dakika ya 45 na Christopher Mepham aliyejifunga dakika ya 51, wakati la Bournemouth limefungwa na 
  Jefferson Lerma .
  Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 55 katika mchezo wa 25, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na Arsenal ambayo pia ina mechi moja mkononi.
  Kwa upande wao, Bournemouth wanabaki na pointi zao 21 za mechi 24 nafasi ya 19.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUMUA BOURNEMOUTH 4-1 VITALITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top