• HABARI MPYA

  Thursday, February 02, 2023

  MAN UNITED YAICHAPA NOTTINGHAM 2-0 NA KUTINGA FAINALI CARABAO


  TIMU ya Manchester United imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Ligi England baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Nottingham Forest katika mchezo wa marudiano usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na Anthony Martial dakika ya 73 na Fred dakika ya 76 wote wakimalizia kazi nzuri za Marcus Rashford.
  Sasa Manchester United watacheza na Newcastle United katika Fainali ya Carabao Cup Februari 26 Uwanja wa Wembley Jijini London.
  Ikumbukwe Newcastle United imepata tiketi ya Fainali baada ya kuitoa ya Southampton FC kwa jumla ya mabao 3-1, ikishinda 1-0 na 2-1 jana Uwanja wa St. James' Park, Newcastle upon Tyne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA NOTTINGHAM 2-0 NA KUTINGA FAINALI CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top