• HABARI MPYA

  Saturday, February 18, 2023

  SIMBA SC YALOWA NYUMBANI, YACHAKAZWA 3-0 NA WAARABU DAR


  WENYEJI, Simba SC wamepoteza mechi ya pili mfululizo ya Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Raja Casablanca ya Morocco leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mshambuliaji Hamza Khaba aliifungia Raja bao la kwanza dakika ya 30, akimalizia pasi ya Mmorocco mwenzake, kiungo Zakaria Habti.
  Naye Soufiane Benjdida akafunga la pili dakika ya 82 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Mmorocco  Mohamed Al Makahasi.
  Aliyehitimisha shangwe za mabao za Raja leo ni beki Mmorocco Ismail Mokadem kwa kufunga la tatu kwa penalti dakika ya 86 kufuatia beki Mkenya, Joash Onyango kuunawa mpira kwenye boksi.
  Raja inafikisha pointi sita na mabao nane ya kufunga bila kuruhusu hata moja ndani ya mechi mbili kufuatia kuilaza Vipers ya Uganda 5-0 kwenye mechi ya kwanza Casablanca.
  Simba SC inakamilisha mechi mbili bila ushindi kufuatia kuchapwa 1-0 na wenyeji, Horoya 1-0 Jijini Conakry nchini Guinea.
  Horoya nayo baada ya sare ya 0-0 leo wenyeji Vipers wanafikisha pointi nne na wanaendelea kukamata nafasi ya pili, wakati Simba inashika mkia.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YALOWA NYUMBANI, YACHAKAZWA 3-0 NA WAARABU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top