• HABARI MPYA

  Saturday, February 11, 2023

  ARSENAL YAAMBULIA SARE KWA BRENTFORD 1-1


  WENYEJI, Arsenal wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Arsenal ilitangulia kwa bao la Leandro Trossard dakika ya 66, kabla ya Ivan Toney kuisawazishia Brentford FC dakika ya 74.
  Kwa matokeo hayo Arsenal inafikisha pointi 51 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu England kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 21. 
  Kwa upande wao, Brentford wanafikisha pointi 34, ingawa wanabaki nafasi ya nane, wakiizidi ponti tatu Chelsea baada ya wote kucheza mechi 22.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAAMBULIA SARE KWA BRENTFORD 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top