• HABARI MPYA

    Thursday, February 16, 2023

    KAMPENI YA MTOKO WA KIBINGWA YATANGAZA WASHINDI WANNE


    DROO ya Kampeni ya Mtoko wa Kibingwa kwa Msimu wa 5  yaibua washindi wanne huku kwa mara ya kwanza  kupatikatika kwaMshindi Mwanamke tangu kuanzishwa kwa Kampeni hiyo.
    Kampuni ya michezo ya ubashiri ya Betika imetangaza washindi wa droo ya kwanza na ya pili kwa Msimu na kupatikana washindi wanne kutoka Mkoani Songea, Simiyu,Kagera pamoja na Dar es salaam. 
    Aidha Mshindi kutoka Mkoa wa Dar es salaam  Mariam  Mohammed mwenye Umri wa miaka 24 kutoka Chamazi amesema anajisikia furaha kushinda katika droo hiyo ya mtoko wa kibingwa kwa Msimu wa 5 akiwa kama Mwanamke. 
    "Nina kawaida ya kucheza mara kwa mara lakini nilipopigiwa na kupewa taarifa kuwa nimeshinda nilifurahi zaidi."
    Hata hivyo Mariam amesema Siku ya Derby hiyo atashangilia timu zote kwani yeye hayupo kwenye timu zote mbili.
    Pia amewashauri wanawake kuweka ubashiri wao kwani michezo ya ubashiri hayachagui jinsia .
    Mshindi kutoka Mkoa wa Ruvuma Songea Constantine Mbele mwenye umri wa miaka 26 anaejihusisha na kazi ya undereva amesema ameshiriki Kampeni hiyo kwa kuweka ubashiri wake kwa shilingi elfu 3000 kwa mikeka 5 yenye mechi 3.
    "Nimeshiriki sana ubashiri kwenye Kampuni ya Betika na nimeshashinda pesa shilingi laki 3 ambayo nilifanya manunuzi ya mbolea ,kununua mahitaji mbalimbali. 
    Aidha Mbele ameeleza shahuku yake kubwa kufika Jijini Dar ambapo hajawahi kufika huku shahuku yake kubwa Kumuona Mchezaji Clotous Chama 
    "Mimi ni shabiki wa Mnyama Simba Aprili 16,2023 natarajia makubwa kwenye timu yangu italeta ushindi dhidi ya Wapinzani wetu Yanga hivyo nategemea zaidi Chama atafunga magoli."
    Pia Msimu huu utachukua washindi 100  na utaenda kukamilisha idadi ya washindi 500 wa Kampeni ya mtoko wa Kibingwa ambapo msimu wa kwanza walishinda washindi 400.
    Kushiriki ubashiri huo ni rahisi kwa kutembelea website www.betika.com au kwa wale wenye viswaswadu kwa kubonyeza *149*16#. Kwa kuweka dau la shilingi mia 500 kwa mikeka mitatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMPENI YA MTOKO WA KIBINGWA YATANGAZA WASHINDI WANNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top