• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2023

  IHEFU SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI


  TIMU ya Ihefu SC imepata ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na washambuliaji wa kigeni, Nelson Okwa dakika ya 40 na Mburkinabe, Yacouba Sogne dakika ya 45, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefumgwa na mzawa, Muhsin Makame dakika ya 62.
  Kwa ushindi huo, Ihefu SC inafikisha pointi 30 na kusogea nafasi ya saba, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 24.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top