• HABARI MPYA

  Saturday, February 04, 2023

  WOLVES YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 MOLINEUX


  WENYEJI, Wolverhampton Wanderers wameiadhibu Liverpool kwa kuichapa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Mabao ya Wolverhampton Wanderers yamefungwa na Joel Matip aliyejifunga dakika ya tano, Craig Dawson dakika ya 12 na Ruben Neves dakika ya 71.
  Kwa ushindi huo, Wolves wanafikisha pointi 20 katika mchezo wa 21 nafasi ya 15, wakati Liverpool wanabaki na pointi zao 29 za mechi 20 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WOLVES YAITANDIKA LIVERPOOL 3-0 MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top