• HABARI MPYA

  Monday, February 27, 2023

  BETIKA KUWALETA DAR KWA NDEGE MASHABIKI KUONA SIMBA NA YANGA


  PROMOSHENI ya Mtoko wa Kibingwa ya Kampuni ya Ubashiri ya Betika, imepata washindi 20,  waliojishindia Tiketi za usafiri wa Ndege (kwenda na kurudi) ili kushuhudia mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Februari 27, 2023, Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa amesema mpaka sasa Washindi 20 wamejishindia tiketi zao za Ndege, pia watashuhudia mchezo huo wa watani wa jadi wakiwa wamekaa kwenye siti maalum (VIP A) katika uwanja huo wa Benjamin Mkapa na kupewa Ulinzi kuelekea uwanjani.
  “Washindi wa Promosheni hii ya Mtoko wa Kibingwa ya Betika, wale wa mikoani watapata fursa kuja Dar es Salaam kwa usafiri wa Ndege (kwenda na kurudi) kwa ajili ya kushuhudia mchezo huo wa kihistoria, pia watakaa siti za VIP A na watasindikizwa na king’ora wakati wanakuja uwanjani na watalala kwenye hoteli ya yenye hadhi ya nyota tano.”
  Amesema mpaka sasa Mabingwa kutoka mikoani waliojishindia ticket za ndege kuja kwenye Mtoko wa Kibingwa ni Bahame Masangwa Balele (Simiyu), Constantine Constantine Mbele (Ruvuma), Stephano Skaut Charles (Kagera), Joshua Charles Gasado (Mkuranga), (Salivius Lucas Frugence (Njombe).
  Washindi wanapatikana kupitia droo za kila wiki huku kila wiki Betika ikitangaza zaidi ya Washindi 10, tarehe ya droo za wiki ni 27, 1, na 3, Machi 2023. Jinsi ya kushiriki kwenye droo, mshiriki anatakiwa kubashiri mikeka mitano, kila siku na hakikisha kila mkeka ana bashiri kwa dau la kuanzia Shilingi 500/- na kuendelea. Pia, mshiriki anaweza kubashiri kupitia Tovuti ya www.betika.co.tz au kwa kupiga *149*16#.
  Hata hivyo, mkeka wako ukichanika au usichanike moja kwa moja mshiriki huyo anaingia kwenye droo ya Mtoko wa Kibingwa ambayo itakupa fursa kuja jijini Dar es Salaam kwa usafiri wa Ndege kushuhudia mtanange wa Simba v Yanga Aprili 16, 2023.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BETIKA KUWALETA DAR KWA NDEGE MASHABIKI KUONA SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top