• HABARI MPYA

  Wednesday, February 08, 2023

  TRY AGAIN WA SIMBA KATIKA KOZI KUBWA YA FIFA


  RAIS wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ baada ya kushiriki moja ya vipindi vinavyoendelea kwenye kozi ya Diploma katika Uongozi wa Klabu inayotolewa na FIFA (Diploma in Club Management) inayofanyika mjini Tangier, Morocco.
  Try Again ni mmoja wa wajumbe watatu kutoka Afrika ambao wanashiriki kozi hiyo ambapo kwa upande wa Afrika Mashariki alichaguliwa yeye peke yake. Huu ni mwendelezo wa FIFA kutoa kozi hiyo kwani ilianzia nchini Qatar wakati Kombe la Dunia likiendelea ambako pia Try Again alishiriki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TRY AGAIN WA SIMBA KATIKA KOZI KUBWA YA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top