• HABARI MPYA

  Sunday, February 05, 2023

  IHEFU SC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 MBARALI


  WENYEJI, Ihefu SC ya Mbarali wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya majirani, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya.
  Mabao ya Ihefu SC yamefungwa na kiungo mahiri, Raphael Daudi Lothi dakika ya 17 na mshambuliaji hatari Adam Adam dakika ya 58.
  Kwa ushindi huo wanafikisha pointi 26 na kusogea nafasi ya nane, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 24 na kushukia nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 MBARALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top