• HABARI MPYA

  Thursday, February 23, 2023

  SIMBA SC YAENDA UGANDA KUSAKA USHINDI KWA VIPERS


  KIKOSI cha Simba SC kimeondoka nchini leo jioni kwenda Uganda kwa ajili ya mchezo wa mwisho mzunguko wa kwanza Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa St. Mary mjini Kitende.
  Zote hazijashinda hata mechi moja katika mbili za awali, Simba ikifungwa 1-0 na Horoya Uwanja wa Jénérali Lansana Conté Jijini Conakry na 3-0 za Raja Casablanca Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wakati Vipers ilitandikwa 5-0 na Raja Jijini Casablanca kabla ya kutoa sare ya 0-0 na Horoya nyumbani, Uganda.  
  Mechi nyingine ya kundi hilo siku hiyo, Raja Casablanca watakokotoana na Horoya kuanzia Saa 4:00 usiku Uwanja wa Mfalme Mohamed wa 5 Jijini Casablanca nchini Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDA UGANDA KUSAKA USHINDI KWA VIPERS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top