• HABARI MPYA

  Wednesday, February 15, 2023

  AZAM YAICHAPA MLANDEGE 3-0 KIRAFIKI CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandege FC katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 52, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 64 na. Cleophace Mkandala dakika ya 90.
  Huo ulikuwa mchezo wa pili kwa kirafiki kwa Azam FC ndani ya wiki moja, baada ya Jumamosi kuichapa KMKM 1-0 hapo hapo Chamazi yote yakiwa maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC Februari 21.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAICHAPA MLANDEGE 3-0 KIRAFIKI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top