• HABARI MPYA

  Thursday, February 09, 2023

  MAN UNITED YAAMBULIA SARE 2-2 KWA LEEDS


  WENYEJI, Manchester United jana wamelazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Leeds United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Leeds United walitangulia kwa mabao ya Degnand Gnonto dakika ya kwanza tu Raphael Varane aliyejifunga dakika ya 48, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Marcus Rashford dakika ya 62 na Jadon Sancho dakika ya 70.
  Kwa sare hiyo Man United inafikisha pointi 43 katika mchezo wa 22, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Manchester City ambao pia wana mechi moja mkononi - wote wakiwa nyuma ya Arsenal yenye pointi 50 za mechi 20.
  Kwa upande wao Leeds United baada ya sare hiyo wanafikisha pointi 19 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya 16, nne tu zaidi ya Southampton inayoshika mkia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAAMBULIA SARE 2-2 KWA LEEDS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top