• HABARI MPYA

  Friday, February 17, 2023

  GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-2 NYANKUMBU


  WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Bashima Sayte dakika ya tano, Geoffrey Manyasi kwa penalti dakika ya 40 na Elias Maguri dakika ya 78.
  Kwa upande wao Ruvu Shooting mabao yao yamefungwa na Abrahman Mussa dakika ya 45 na Mgandila Shaaban dakika ya 63.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 34 nafasi ya tano, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 17 nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA RUVU SHOOTING 3-2 NYANKUMBU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top