• HABARI MPYA

  Sunday, February 19, 2023

  MANCHESTER UNITED YAICHAPA LEICESTER CITY 3-0 OLD TRAFFORD


  WENYEJI, Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Mabao ya Manchester United yamefungwa na mshambuliaji aliye katika kiwango kizuri mno, Marcus Rashford mawili dakika ya 25 na 56 na Jadon Sancho dakika ya 61.
  Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 49, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa pointi tatu na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Leicester City inabaki na pointi zake 24 za mechi 23 nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER UNITED YAICHAPA LEICESTER CITY 3-0 OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top