• HABARI MPYA

  Wednesday, February 22, 2023

  REAL MADRID YAIFUMUA LIVERPOOL 5-2 ANFIELD


  NYOTA Mbrazil, Vinícius Júnior na mkongwe wa Ufaransa, Karim Benzema kila mmoja jana alifunga mabao mawili kuiwezesha Real Madrid kutoka nyuma na kushinda 5-2 dhidi ya wenyeji, Liverpool katika mchezo wa kwanza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Anfield Jijini Liverpool.
  Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uruguay, Darwin Nunez alianza kuifungia Liverpool dakika na nne na nyota wa Misri, Mohamed Salah akafunga la pili dakika 10 baadaye.
  Real wakazinduka kwa mabao ya Vinícius Júnior dakika ya 21 na 36, 47' Éder Militão dakika ya 47 na  Benzema dakika ya 55 na 67.
  Timu hizo zitarudiana Machi 15 Uwanja wa Santiago Bernabéu Jijini Madrid na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAIFUMUA LIVERPOOL 5-2 ANFIELD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top