• HABARI MPYA

  Saturday, February 11, 2023

  CHELSEA YAAMBULIA SARE 1-1 NA WEST HAM LONDON


  WENYEJI, West Ham United wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Chelsea FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa London Jijini London.
  Nyota Mreno, Joao Felix alianza kuwafungia wageni, Chelsea dakika ya 16, kabla ya Emerson kuwasawazishia Wagonga Nyundo wa London dakika ya 28.
  Kwa matokeo hayo, West Ham United inafikisha pointi 20, ingawa inabaki nafasi ya 16, wakati Chelsea sasa una pointi 31 na inasogea nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 22.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAAMBULIA SARE 1-1 NA WEST HAM LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top