• HABARI MPYA

  Sunday, February 26, 2023

  S4C YA BETIKA YAENDELEA KUSHIKA KASI COCO BEACH


  MASHUNDANO ya Sodo 4 Climate (S4C) ya Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Betika kwa kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust imeendelea kushika kasi katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam, huku lengo la mashindano hayo ikiwa ni kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira.
  Katika michezo iliyochezwa Jumamosi ya Februari 25, 2023 katika viwanja hivyo, ilishuhudiwa timu za Sodo upande wa Wanaume na Wanawake za Friends of Tulia Trust zikiaga mashindano hayo. Timu ya Wanawake ya Tulia ilichapwa mabao 1-2 na timu ya Espanyol huku timu hiyo ya Friends of Tulia Trust ya Wanaume ikipigwa mabao 0-2 dhidi ya timu ya Espanyol.
  Mnamo Machi 4, 2023 mashindano hayo yataendelea ambapo timu ya Mkuu wa Mkoa, RC FC itamenyana na timu ya Bodaboda FC ya Msasani katika viwanja hivyo vya Coco Beach, jijini Dar es Salaam.
  Mashindano hayo ya Ligi ya Betika (Sodo 4 Climate) yanafanyika katika viwanja hivyo vya Coco Beach yakiwa na lengo mahsusi kusaidia utunzaji wa mazingira, sanjari na kushirikiana na wadau wengine kama Taasisi ya Tulia Trust (Friends of Tulia Trust Foundation).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: S4C YA BETIKA YAENDELEA KUSHIKA KASI COCO BEACH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top