• HABARI MPYA

  Saturday, February 11, 2023

  AISHI AOKOA PENALTI SIMBA YACHAPWA 1-0 GUINEA


  TIMU ya Simba SC imeanza vibaya mechi zake za Kundi C Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Horoya AC leo Uwanja wa Jenerali Lansana Conte Jijini Conakry nchini Guinea.
  Bao pekee la Horoya leo limefungwa na mshambuliaji kinda wa miaka 21, Msenegal Pape Abdou N'Diaye dakika ya 18 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Niger, Amadou Djibo Mohamed Wonkoye.
  Pape N'Diaye aliikosesha Horoya nafasi ya kupata bao la pili baada ya mkwaju wake wa penalti kuokolewa na kipa namba moja Tanzania, Aishi Salum Manula dakika ya 73 kufuatia beki Mkenya, Joash Onyango kuunawa mpira kwenye boksi.  
  Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Raja Casablanca ilishinda 5-0 dhidi ya Vipers ya Uganda Uwanja Mfalme Mohamed V Jijini Casablanca nchini Morocco.
  Mechi zijazo, Simba watakuwa wenyeji wa Raja Casablanca Dar es Salaam na Vipers watakuwa wenyeji wa Horoya mjini Entebbe nchini Uganda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AISHI AOKOA PENALTI SIMBA YACHAPWA 1-0 GUINEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top