• HABARI MPYA

  Friday, February 24, 2023

  MAN UNITED YAICHAPA BARCELONA 2-1 EUROPA LEAGUE

   


  WENYEJI, Manchester United wamefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora michuano ya UEFA Europa League baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Barcelona usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.
  Lakini haukuwa ushindi mwepesi kwao, kwani Mashetani Wekundu walilazimika kutoka nyuma baada ya Robert Lewandowski kuitanguliza Barca kwa bao la penalti dakika ya 18 kufuatia Bruno Fernandes kumchezea rafu Alejandro Balde kwenye boksi ambayo ilibidi refa Mfaransa, Clement Turpin apate msaada wa VAR kufanya maamuzi.
  Lakini Manchester United ikazinduka kwa mabao ya Wabrazil wawili, kiungo Fred dakika ya 47 na Antony dakika ya 73 na kukata tiketi ya Hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 4-3 kufuatia sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Barcelona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA BARCELONA 2-1 EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top