• HABARI MPYA

  Saturday, February 11, 2023

  MTIBWA SUGAR DODOMA JIJI FC 2-1 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar leo yamefungwa na Vitalis Mayanga dakika ya 30 na Charles Ilanfya dakika ya 61, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Seif Abdallah Karihe dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya saba, wakati Dodoma Jiji FC inabaki na pointi zake 24 nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi 23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR DODOMA JIJI FC 2-1 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top