• HABARI MPYA

  Saturday, February 18, 2023

  MAN CITY YAACHIA USUKANI ENGLAND


  MABINGWA watetezi, Manchester City wameachia usukani wa Ligi Kuu ya England baada ya kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Nottingham Forest leo Uwanja wa The City Ground Jijini Nottingham, Nottinghamshire.
  Manchester City ilitangulia na bao la Bernardo Silva dakika ya 41 akimalizia pasi ya Jack Grealish, kabla ya C. Wood kuisawazishia Nottingham Forest dakika ya 84 akimalizia kazi nzuri ya M. Gibbs-White.
  Kwa matokeo hayo, Manchester City inafikisha pointi 52 katika mchezo wa 24 na kushukia nafasi ya pili ikiipisha tena kileleni Arsenal yenye pointi 54 za mechi 23, wakati Nottingham Forest inafikisha pointi 25 za mechi 23 pia nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY YAACHIA USUKANI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top