KIKOSI cha Yanga kimeondoka leo nchini kwenda Bamako nchini Mali kwa ajili ya mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Réal Bamako Jumapili kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Machi 26 Jijini Bamako.
Mechi nyingine ya kundi hilo Jumapili; TP Mazembe watakuwa wenyeji wa Monastir ya Tunisia kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa TP Mazembe Jijini Lubumbashi, DRC.
0 comments:
Post a Comment