• HABARI MPYA

  Friday, February 10, 2023

  SIMBA QUEENS YAPANDA KILELENI LIGI YA WANAWAKE


  HATIMAYE mabingwa watetezi, Simba SC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara baada ya Raundi nane.
  Kufuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Bao Bab Queens jana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Simba sasa inaongoza ligi kwa pointi moja zaidi ya JKT Queens waliouanza vizuri msimu na kukaa kileleni kwa mida mrefu.
  Simba Queens ina pointi 19, ikifuatiwa na JKT pointi 18, watani wa jadi Yanga Princess pointi 17 sawa na Fountain Gate Princess baada ya timu zote kucheza mechi nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YAPANDA KILELENI LIGI YA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top