• HABARI MPYA

  Tuesday, February 21, 2023

  SIMBA SC YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE NA AZAM FC 1-1


  WENYEJI, Simba SC wameambulia sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Azam FC walitanguli na bao la dakika ya kwanza tu la mshambuliaji wake wa Kimataifa wa Zimbabwe. Prince Dube Mpumelelo, kabla ya beki Mzanzibari Abdallah Kheri ‘Sebo’ kujifunga dakika ya 90 na ushei kuipa bao la kusawazisha Simba.
  Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 54 na kuendelea kushika nafasi ya pili ikiizidi pointi 10 Azam FC baada ya wote kucheza mechi 23, wakiwa nyuma ya Mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 59 za mechi 22.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO KUPATA SARE NA AZAM FC 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top